Usajili wa wakulima wanukia

0
141

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema usajili wa alama za vidole kwa wakulima unakaribia kuanza, lengo likiwa ni kupata takwimu sahihi za idadi ya wakulima nchini.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa maonesho na sherehe za sikukuu ya wakulima (Nanenane) kitaifa zinazoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa Waziri Bashe, serikali inahitaji kutenga ruzuku za kilimo zinazoendana na idadi sahihi ya wakulima nchini na kwamba vifaa kwa ajili ya kazi ya usajili tayari vimekwishaandaliwa.

Pia ametumia ufunguzi wa maonesho hayo kuwasihi wakulima nchini kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

Amesema sensa ni njia mojawapo ya kuwatambua wakulima na aina ya mazao wanayolima.

Maonesho na sherehe za sikukuu ya wakulima (Nanenane) kitaifa zilizozinduliwa hii leo zitafikia kilele chake tarehe 8 mwezi huu.