Upigaji kura waendelea katika maeneo mbalimbali nchini

0
244

Zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Upigaji kura ulianza Saa Mbili kamili asubuhi na unatarajiwa kukamilika saa Kumi jioni.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), watu wote watakaokuwa kwenye mistari ya kupiga kura hadi saa Kumi jioni, zoezi hilo litaendelea mpaka hapo watakapomalizika.

Tayari TAMISEMI imetangaza kuwa, uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa hautafanyika katika mikoa ya Njombe, Tanga, Katavi na Ruvuma, baada ya Wagombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupita bila kupingwa.