Upatikanaji maji Dar 100 %

0
59

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam imerejea kwa asilimia mia.moja, baada ya kuwepo kwa mgawo kufuatia hali ya ukame katika mto Ruvu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema, kwa sasa lita milioni 590 zinazalishwa kwa siku kutoka lita milioni 300 kwa siku zilizokuwa zikizalishwa wakati wa ukame.

Mhandisi Luhemeja amesema DAWASA inaendelea na mikakati ya kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wakazi wa maeneo ambayo hawajafikiwa na huduma hiyo ndani ya mkoa wa Dar es Salaam likiwemo eneo la Ukonga.