Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania TPA imesema ipo katika hatua za mwisho za kuanza awamu ya pili ya ujenzi na upanuzi wa bandari ya Kagunga iliyopo kaskazini mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.
Mkurugenzi mkuu wa Tpa mhandisi Deusdedit Kakoko upanuzi huo wa bandari ya Kagunga utasaidia kurahisisha biashara kwa nchi za mwambao wa ziwa Tanganyika na kudhibiti mianya ya utoroshaji wa bidhaa.
Amesema kuwa kazi hiyo ambayo pia itahusisha na uendelezaji wa ujenzi wa soko la ujirani mwema Kagunga itaanza mwanzoni mwa mwezi janury mwaka 2019.
Tayari gati na majengo ya kisasa vimekamilika, ishara ya kuelekea hatua za mwisho za ujenzi wa bandari hii inayoelezwa kuwa ya kipekee kutokana na kuwa na eneo kubwa lenye kina cha maji cha kutosha kwa ajili ya kuhudumia meli.
