Uongozi ni Dhamana si Zawadi

0
133

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi ambao amekuwa akiwateua wajue kuwa uongozi ni dhamana na si zawadi.

Amesema hatarajii kuona Viongozi anaowateua wanakuwa Miungu watu, bali anachotaka Viongozi hao wajielekeze katika kuwatumikia Wananchi.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.

Amewataka Viongozi hao kuwa mfano wa kuigwa ndani ya jamii na kuzingatia miiko ya uongozi.

Hafla ya kuwaapisha Viongozi hao imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma.