Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Fabian Daqqaro amewaomba wakazi wa kata ya Moivaro eneo la Moshono jijini Arusha kuwa watulivu wakati jitihada za kufukua kifusi zikiwa zinaendelea, kufuatia watu Watatu pamoja na gari lililokuwa likipakia Moramu kufukiwa na kifusi.
Akizungumzia tukio hilo, Daqqaro amesema kuwa limetokea majira ya saa moja asubuhi hii leo, ambapo majeruhi Wawili wanapatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Arusha, – Mount Meru.
Amesema kuwa kazi inayoendelea hivi sasa, ni kutafuta vifaa mbalimbali vitakavyoweza kuongeza nguvu katika kazi ya uokoaji inayoendelea hivi sasa.