UNFPA yaungana na Polisi Mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia

0
161

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Jamii imeanza kuelewa madhara yatokanayo na ukatili wa kijinsia baada ya kupata elimu ya kutosha ya dhidi ya vitendo hivyo.

IGP Simon Sirro ametoa kauli hiyo wakati akipokea msaada wa pikipiki 10 zenye thamani ya zaidi ya milioni 51.3 zilizotolewa na UNFPA Jijini Dar es Salaam ambazo zitapelekwa mikoani kusaidia mapambano ya ukaliti wa kijinsia.

Kamanda Sirro amesema bado tatizo halijadhibitiwa kabisa na hivyo kutoa wito kwa jamii kuacha tabia hiyo kwakuwa jeshi la polisi lipo macho na litawakamata wote watakao bainika kufanya vitendo hivyo.

“Nawashukuru Sana UNFPA kwa msaada wa pikipiki hizi, tunaamini zitasaidia Sana kupambana na wanaofanya ukali huo huku nikiwakumbusha kuwa hata ukeketaji sisi tunachukulia kama shambulio la kimwili na Kuna adhabu zake Kali” ameongeza IGP Sirro

Kwa upande wake meneja wa operesheni za Kimataifa wa UNFPA Tanzania Georgette Kyomba amesema, msaada huo wa pikipiki utasaidia madawati ya kijinsia kukabiliana na ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto na wataendelea kutoa kila ushirikiano Katika kukabiliana na ukatili hapa Nchini