Unapokwenda popote umeibeba Tanzania mgongoni

0
152

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika hafla ya uapisho wa Mabalozi aliowateua hivi karibuni Ikulu Chamwino mkoani Dodoma amesema, Mabalozi wanapaswa kufahamu kuwa wameibeba Tanzania mgongoni mwao wanapokuwa katika vituo vyao vya kazi.

“Unapokwenda popote ujue umeibeba Tanzania mgongoni kwako, mambo yote ya Tanzania yanayotokea pale ni juu yako, kwa hiyo nawaonbeni sana muende mkiwa mnalifahamu hilo na mnalizingatia hilo.” Amesema Rais Samia

Ameongeza kuwa katika maeneo wanayokwenda Mabalozi hao yapo masuala ya kikanda, hivyo wanapaswa kufahamu kuwa wanaiwakilisha Tanzania kwenye masuala hayo ya kikanda na yale ya kimataifa yakiwemo na ya ndani ya nchi.

Aidha, Rais Samia amesema mambo au maneno watakayoyazungumza huko, huo ndio msimamo wa Rais na ndio msimamo wa Taifa la Tanzania na ikiwa watafanya kinyume hayo ni yao ambapo yatalifaidisha Taifa au kulifedhehesha Taifa.