Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limeaswa kuendeleza dhana ya ushirikishwaji wa wafanyakazi mahala pa kazi ili kufikia uelewa na maamuzi ya pamoja.
Akitoa elimu ya umuhimu wa baraza la wafanyakazi kwa baraza hilo Afisa Elimu Kazi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Emiliana Rweyendela amesema yapo manufaa makubwa ya ushirikishwaji wa wafanyakazi katika mahala pa kazi hivyo ni jambo linalopaswa kupewa uzito.
Moja ya manufaa hayo ameyataja kuwa ni kuwaongezea ari ya kufanya kazi watumishi, kuwapa motisha katika kazi pamoja na kufikia uelewa na maamuzi ya pamoja.
Baraza jipya la wafanyakazi la TBC limekutana leo kwa lengo la kujadili bajeti ya shirika, maazimio ya hoja mbalimbali za wafanyakazi na mwelekeo wa shirika hilo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.