Umbali wa magereza wachelewesha usikikizwaji wa kesi

0
165

Jaji Mkuu wa Tazania, Prof. Ibrahim Hamis Juma amezishauri wilaya kujenga magereza ya wilaya ili kuwezesha mahabusu kuwa karibu na mahakama.

Amesema hatua hiyo itaongeza kasi ya usikilizaji wa kesi kwa kuwa mahabusu wengi watakuwa wanahudhuria mahakamani.

Prof. Juma ameeleza hayo kwenye kikao kati ya Tume ya Utumishi wa Mahakama na wajumbe wa kamati za maadili za mkoa wa Iringa kilichofanyika mjini humo.

Kwa majibu wa Jaji Mkuu, idara ya mahakama inatarajia kujenga mahakama za wilaya kwenye wilaya 25 nchini lakini changamoto kubwa ni uchache wa mahabusu zilizopo na umbali zilipo.

“Endapo kila wilaya itajenga gereza basi mahabusu watakuwa karibu na kila siku kesi zitasikilizwa tofauti na hali ilivyo sasa,” amesema Jaji Mkuu.