Ulivyokuwa usiku wa Sensa kiwanda cha Dangote

0
109

Saa sita na dakika moja usiku wa kuamkia hii leo zoezi la sensa ya Watu na Makazi lilianza katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo mkoani Mtwara lilifanyika katika maeneo kadhaa ikiwemo kiwanda cha saruji cha Dangote.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dustan Kyobya akiwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Thomas Salasala walifika katika kiwanda hicho kuhakikisha wafanyakazi zaidi ya 3,000 wa kiwanda hicho wanahesabiwa.