Ulinzi Kuimarishwa nchini Tanzania

0
394

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini vimejipanga kuhakikisha vinadhibiti vitendo vya uhalifu hasa kutokana na vitendo vya vurugu vinavyoendelea katika nchi jirani ya Msumbiji. 

IGP Sirro amesema hayo wakati akizungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi, nakuwataka wananchi kujikita katika shughuli halali za kujiletea maendeleo.

Aidha, amewataka Watanzania hususan vijana kuacha kutumiwa na watu wachache  wanaowataka wajiingize kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani nchini ikiwemo kufanya uhalifu.