Ulega: Tanzania ni salama kwa uwekezaji

0
118

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewahakikishia mazingira mazuri na ya uhakika Wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta ya ufugaji na uvivu.

Waziri Ulega ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika, unaojumuisha wadau wa chakula kutoka Barani Afrika na nje ya bara hilo.

Amesema Tanzania ina eneo kubwa kwa ajili ya ufugaji, hali ya hewa nzuri pamoja miundombinu ya kufaa kwa ajili ya uwekezaji kwenye sekta hiyo ya mifugo.

Aidha, Waziri Ulega amesema Serikali inaendelea na jitihada zake za kuwawezesha wawekezaji wa ndani na kuboresha mifumo ya ufugaji hasa kwa Wanawake na Vijana ili kuwawezesha kufuga kwa ufanisi.