Ukosefu wa ‘barcode’ wakwamisha soko la bidhaa

0
308

Kukosekana kwa msimbomilia (barcode) kwenye bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa hapa nchini ni miongoni mwa changamoto zinazosababisha bidhaa hizo kukosa masoko ya ndani na kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 10, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utoaji Msimbomilia (GS1), Jumbe Menye amesema ni muhimu elimu ikaendelea kutolewa kwa wajasiriamali na wenye viwanda ili kuwawezesha kupata masoko.

Kwa kutambua changamoto hiyo kubwa, GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Viwanda (TIRDO) na taasisi ya kusaidia wajasiriamali ya Guru Planet wameadaa siku maalumu iliyopewa jina la Prime Ministers Bar Code Day itakayofanyika Machi 21 ikiambatana na maonesho ya wajasiriamali yatakayoanza Machi 17 hadi Machi 21. Mgeni rasmi atakua Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1, Fatma Kange na Mwakilishi wa TIRDO, Purifiketa Andrew wamesema ni muhimu elimu ikaendelea kutolewa na utafiti kufanyika ili lengo la uchumi wa viwanda liweze kifikiwa.