Ukaguzi wa maduka yakubadilishia fedha waimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania

0
635

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema kuwa ukaguzi
katika maduka ya kubadilisha fedha uliofanyika kwenye baadhi ya mikoa
nchini, umesaidia kuimarisha thamani ya Shilingi ya Tanzania na upatikanaji wa fedha za kigeni katika benki za biashara.

Dkt Mpango ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari na kuongeza kuwa kabla ya ukaguzi huo Dola Moja ya Kimarekani ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 2,450 na baada ya ukaguzi huo kwa sasa Dola inauzwa kwa wastani wa Shilingi 2,300.