Ujumbe wa Uganda wawasili Tanga

0
123

Ujumbe wa watu 26 kutoka Nchini Uganda ukiongozwa na Waziri wa Nishati wa Nchi hiyo Peter Lokeri umewasili mkoani Tanga lengo likiwa ni kujionea maendeleo ya mradi wa Bomba la Mafuta linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda kuja Tanga Tanzania.

Miongoni mwa viongozi walioambatana na wageni hao ni pamoja na Balozi wa Uganda nchini Tanzania Richard Kabonero, katibu mkuu wa wizara ya Nishati mhandisi Felichesmi Mramba na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge Nishati Dustan Kitandula, mwenyekiti kamati ya bunge uwekezaji viwanda na mazingira Issa Mchungahela.

Mbali na eneo la Chongoleani eneo lingine ambapo shughuli za mradi wa bomba la mafuta zinaendelea kwa sasa ni eneo la Sojo wilayani Nzega mkoani Tabora ambapo panajengwa karakana ya kupakwa rangi mabomba kuweka mfumo wa kuzuia joto lisipotee.

Ugeni huo upo hapa nchini kwa muda wa wiki sita.