Ujumbe wa Japan waitembelea TBC

0
219

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Martha Swai amesema kuwa, ushirikiano baina ya Japan na TBC, umesaidia katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa baadhi ya studio za Shirika hilo.

Swai amesema hayo baada ya kupokea ujumbe kutoka Japan, ukiongozwa na Balozi wa nchi hiyo hapa nchini Shinichi Goto.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa TBC, – Upendo Mbele amemuomba Balozi Goto kuhuisha ushirikiano wa ubadilishanaji Watumishi katika Idara ya ufundi ili kupata ujuzi katika Teknolojia ya kisasa.

Naye Balozi Goto amesema kuwa, Japan kupitia Shirika lake la Utangazaji (NHK), itaendelea kushirikiana na TBC ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Shirika hilo.