Ujenzi wa Kongani kubwa ya viwanda sasa rasmi

0
253

Hatimaye kitendawili cha ardhi kwa ajili ya Mwekezaji wa Kongani kubwa ya viwanda Kigamboni mkoani Dar es Salaam kimeteguliwa, baada ya Serikali kumkabidhi Mwekezaji wa Kongani hiyo Kampuni ya Elsewedy Electric ardhi yenye ukubwa wa square mita milioni 2.8 kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema tukio la Mwekezaji huyo kukabidhiwa ardhi ya kuanza ujenzi huo, Tanzania inaenda kuandika historia mpya ya kuwa na Kongani kubwa tangu Uhuru na kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kongani hiyo itakuwa na viwanda 100 katika sekta mbalimbali, na kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Profesa Godious Kahyarara, kon…