Ujenzi wa Ikulu Dodoma wamkosha JPM

0
651

Rais Dkt John Magufuli amekagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Ikulu mkoani Dodoma na kuelezea kuridhishwa na ujenzi huo.

Ujenzi wa ofisi hizo unaofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),
ulianza Februari 17 mwaka huu na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 3 ijayo.

Msimamizi wa ujenzi wa ofisi hizo za Ikulu mkoani Dodoma Luteni Kanali George Nyisa, amemueleza Rais Magufuli kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati uliopangwa.

Akikagua majengo ya ofisi hizo, Dkt Magufuli amefurahishwa na uimara wa nguzo na kuta zinazojengwa na amesema ni fahari kubwa kwa Taifa kujenga ofisi yake ya Ikulu kwa kutumia Jeshi badala ya kutumia wakandarasi kutoka nje ya nchi.

Rais Magufuli pia amezungumza na Vijana wa JKT wanaoshiriki ujenzi huo na kuwakumbusha ahadi yake kuwa vijana hao 2,424 wataandikishwa JWTZ mara watakapomaliza jukumu la ujenzi wa ofisi za Ikulu.

Pia amewapongeza vijana wa kiraia wanaoshiriki katika ujenzi huo ambao ni mafundi, na amewaahidi kuwa atawaangalia mara baada ya kumaliza kazi hiyo.

Ujenzi wa ofisi za Ikulu mkoani Dodoma,
unafanywa kwa usanifu na muonekano sawa na ofisi za Ikulu zilizopo jijini Dar es salaam.