Ujenzi wa Chelezo katika bandari ya Mwanza waendelea vizuri

0
137

Ujenzi wa Chelezo katika bandari ya Mwanza umefikia asilimia 55, na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwaka 2020.

Hadi kukamilika kwake ujenzi huo utakuwa umegharimu Shilingi Bilioni 36.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa ujenzi huo wa Chelezo katika bandari ya Mwanza Mhandisi Paul Olekashe amesema kuwa, ujenzi huo ulianza mwezi Machi mwaka huu.

Chelezo hiyo ambayo itakua kubwa katika Ziwa Viktoria, itakuwa na uwezo wa kubeba Tani Elfu Nne.

Kampuni ya STX Engine kutoka Korea Kusini ndiyo iliyopewa kazi ya kujenga Chelezo hiyo katika Bandari ya Mwanza.