Ujenzi wa barabara ya Nyamazobe – Mlimani waendelea

0
731

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), -Selemani Jafo ameelezea kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Nyamazobe – Mlimani wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, barabara iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi na baadaye kuungwa mkono na serikali.

Akikagua ujenzi huo, Waziri Jafo ameuagiza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) mkoani Mwanza kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kabla ya mwezi Aprili mwaka huu.

Mratibu wa TARURA mkoani Mwanza, -Koyoyo Fuko amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 2 Nukta 5 umekamilika kwa asilimia 80.

Katika kuunga mkono jitihada za Wakazi wa Nyamazobe – Mlimani za kujenga barabara hiyo, uongozi wa wilaya ya Nyamagana umechangia Shilingi Milioni Thelathini na Rais John Magufuli  amechangia Shilingi Milioni Ishirini.