Pori la akiba la Selous bado linakabiliwa na changamoto ya ujangili ambapo kwa mwaka 2016/2017 jumla ya kesi 92 zilifunguliwa, zilizoripotiwa na mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori nchini (TAWA).
Akizungumza na vyombo vya habariĀ mkuu wa pori hilo kanda ya kaskazini magharibi Augustino Ngimilanga amesema sababu kubwa ya kuwepo kwa changamoto hiyo ni muingiliano kati ya wananchi na hifadhi.