Uingizwaji wa dawa za kulevya nchini wapungua kwa asilimia 90

0
127

Rais John Magufuli amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wa awamu ya tano, serikali.imefanikiwa kudhibiti uingizwaji nchini wa dawa za kulevya kwa asilimia 90.


Akifunga Bunge la 11 la jijjni Dodoma, Rais Magufuli amesema katika kipindi hicho zaidi ya watuhumiwa elfu 37 wa biashara ya dawa za kulevya wamekamatwa.


Ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya Nchini kwa kufanya kazi nzuri katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.


Amesema kuwa jitihada zilizofanywa na Mamlaka hiyo pamoja na serikali, ndizo zilizolifanya Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na udhibiti wa dawa za kulevya na uhalifu kuipongeza Tanzania kufuatia mafanikio iliyoipata katika kudhibiti uingizaji wa dawa za kulevya.


Rais Magufuli pia amewapongeza wabunge wa Bunge hilo la 11 ambalo limemaliza muda wake kwa kutunga sheria nzuri ambazo zimesaidia katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, pamoja na Wananch