Wanasayansi wamefichua uhusiano kati ya kunywa maji ya kutosha na kuzeeka
ambapo unywaji maji kwa usahihi unaweza kupunguza kasi ya uzee na kuongeza maisha bila ya magonjwa.
Ni ukweli usiopingika kwamba kunywa maji kuna manufaa kwa afya zetu. Mbali na mchango wake katika mwili wa kimetaboliki, pia yana jukumu muhimu la kuipa ngozi ya mwanadamu unyevu.
Kulingana na utafiti mpya wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya (NIH) nchini Marekani maji ya kunywa yanahusisha uzee wenye afya na unywaji mzuri wa maji.
Kulingana na tafiti hizo, watafiti waliangalia uhusiano kati ya dalili kadhaa za kiafya na viwango vya chumvi chumvi katika damu, ambavyo huongezeka wakati unywaji wa maji umepungua.
Utafiti huo umejumuisha taarifa za kiafya zilizopatikana kutoka kwa washiriki 11,255 katika kipindi cha miaka 30.
Kwa upande mwingine watafiti hao wamegundua kuwa, watu wazima walio na kiwango cha juu ya wastani cha Sodium katika majimaji ya damu walikuwa na uwezekano mkubwa wakupata magonjwa sugu kulinganisha na wale wenye kiwango cha wastani. Hivyo watu wazima walio na viwango vya juu vya sodium walikuwa na hatari kubwa ya kupoteza maisha mapema zaidi.
“Matokeo yanaonesha unywaji sahihi wa maji unaweza kupunguza kasi ya kuzeeka na kurefusha maisha bila ya kupata magonjwa,” alisema Natalia Dmitrieva, Ph.D., Mwandishi wa utafiti na mtafiti katika taasisi ya Tiba ya Moyo, Mapafu na Damu (NHLBI).
Utafiti huu unatokana na utafiti wa awali ulioanza kufanyika tangu mwaka 1987 ambao ulichapishwa Machi 2022 iligundulika uhusiano kati ya viwango vya kawaida vya sodiamu na uwezekano mkubwa wa moyo kushindwa kufanya kazi.
Matokeo ya tafiti hizo yalitoa tathmini ya viwango vya sodium kwa kueleza kuwa watu walio na viwango vya kawaida vya sodium katika seramu ya zaidi ya mililita 135 hadi 146 kwa lita (mEq/L) walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuonesha viashiria vya uzee wa kibaiolojia kwa kasi zaidi.
Hivyo tafiti hii inatafsiri kuwa watu hao wana uwezekano mkubwa wakuzeeka kwa haraka zaidi.