UHARIBIFU WA MAZINGIRA WILAYANI MBOZI WAMNYIMA USINGIZI MGUMBA

0
130

Mkuu Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amekasirishwa na vitendo vya uharibifu wa Mazingira vinavyofanywa na baadhi ya wananchi katika misitu ya LongSort iliyopo kata ya Hasamba Wilayani Mbozi

Mgumba ambaye yuko kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani Mbozi amesema uharibifu unaofanywa katika misitu hiyo hauvumiliki hata kidogo.

Ameongeza kuwa kama uharibifu huo utaendelea kwa viwango hivo basi hakuna haja ya kuwa na Viongozi kuanzia ngazi ya kijiji ambao wanaona uharibifu unaendelea hawachukui hatua zozote za kisheria

Hata hivo Mgumba ameagiza jeshi la Polisi Mkoani humo kuwakamata watu Tisa wanaodaiwa kuwa wanaharibu Mazingira kwa kuchoma Mkaa bila kuwa na kibali.