Uhaba wa Dola wapandisha bei za mafuta

0
195

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa mwezi Agosti, 2023 kuanzia leo.

Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yamesababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na changamoto ya upatikanaji wa Dola za Kimarekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya Dola ya Kimarekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uingizaji wa mafuta nchini.

Kufuatia mabadiliko hayo, bei za rejareja kwa mkoa wa Dar es Salaam Petroli ni shilingi 3, 199 kwa lita, dizeli shilingi 2,935 kwa lita na
mafuta ya taa shilingi 2, 668 kwa lita moja.

Mkoani Tanga petroli inauzwa shilingi 3, 245, dizeli shilingi 2, 981 na mafuta ya taa yanauzwa kwa shilingi 2, 740 kwa kila lita moja huku kwa mkoa Mtwara petroli yenyewe inauzwa kwa shilingi 3, 271, dizeli shilingi 3, 008 na mafuta ya taa shilingi 2, 714 kwa lita.

EWURA imewataka Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta wanaouza kwa rejareja kuuza mafuta kwa bei zilizoainishwa na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka bei hizo.