Uganda yatangaza mlipuko wa Ebola

0
137

Serikali ya Uganda imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini humo.

Mlipuko huo wa Ebola umetangazwa nchini Uganda baada ya mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 24 kufariki dunia baada ya kuugua ugonjwa huo.

Maafisa wa Afya nchini Uganda wamesema, kijana huyo alithibitika kuwa na dalili zote za Ebola.

Wamesema kijana huyo aliyefariki dunia baada ya kuugua Ebola ni mkazi wa kijiji cha
Ngabano kilichopo katka wilaya ya Mubende.