Ufaulu wa mtihani wa Darasa la Saba waongezeka kwa asilimia 3.78

0
197

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Septemba 11 na 12 mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo kwa Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt Charles Msonde amesema kuwa, asilimia 81.50 ya Watahiniwa 933,369 waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Amesema kuwa katika mtihani huo, Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo yao kwa sababu ya udanganyifu.

Kwa mujibu wa Dkt Msonde, matokeo ya jumla yanaonyesha kwa mwaka huu ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78 ikilinganishwa na mwaka 2018.