Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka 2023 yanayoonesha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka 2022.
Akitangaza matokeo hayo huko Zanzibar, Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Said Mohamed amesema, watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 106, 883, wasichana 47, 340 na wavulana 59, 543.
Amesema watahiniwa 104,549 sawa na asilimia 99.23 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo wa kidato cha sita mwaka 2023 wamefaulu.
Wasichana waliofaulu ni 46,707 sawa na asilimia 99.51 huku kwa upande wa wavulana, waliofaulu ni 57, 843 sawa na asilimia 99.
Mwaka 2022 waliofaulu walikuwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka 2023.