Balozi wa Ufaransa nchini, – Frederic Clavier ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jitihada zake za kuliletea Taifa maendeleo pamoja na Wananchi wake.
https://www.youtube.com/watch?v=644FbENrv5A
Balozi Clavier ametoa pongezi hizo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Rada Mbili za kuongozea ndege katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ambapo pia ametumia lugha ya kiswahili kutoa pongezi hizo.