UDSM: Mahafali yasitishwa kuomboleza kifo cha Rais mstaafu

0
212

Kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kimesitisha duru ya kwanza ya mahafali ya 50.

Kufuatia tangazo lililotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. William Anangisye, mahafali hayo yalipangwa kufanyika leo, Julai 24 saa 12: 30 mchana katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.

Chuo kimeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wahitimu, wadau na umma kwa ujumla na mahafali yatafanyika hapo itakapo tangazwa tena.