Udhibiti sekta ya madini wachochea bidii kwa wachimbaji

0
266

Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema kuwepo kwa udhibiti na uwazi katika sekta ya madini kumechochea wachimbaji kujituma na kufuata taratibu zilizowekwa na serikali.

Biteko amezungumza hayo katika mahojiano maalum na TBC Aridhio na kueleza kuwa kwa sasa hakuna faida ya kutorosha madini kwa sababu mifumo yote ya kiulinzi ipo ikiwemo kujengwa kwa ukuta Mererani.

Ameongeza kuwa uwepo wa masoko ya madini kumewanufaisha wachimbaji kwani wanauza madini kwa bei nzuri kulingana na sheria iliyowekwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko amejibu uvumi unaoenea kuhusu bei halisi ya madini yaliyonunuliwa hivi karibuni kutoka kwa mchimbaji mdogo, Saniniu Laizer, na kusema kuwa serikali haiwezi kumpunja mwananchi wake kwani kabla ya kununuliwa zoezi la kutathmini thamani ya madini hayo lilifanyika.

Kuhusu madini hayo na mpango wa kuwekwa makumbusho, Biteko amesema serikali itakuja na taarifa rasmi ya namna yatakavyotumika ili yaweze kuliingizia Taifa mapato.