Uchimbaji madini kwenye maeneo ya misitu kuangaliwa

0
183

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini – TFS Profesa DOS SANTOS SILAYO amesema kuwa, kuanzia sasa Wakala huo hautaruhusu uchimbaji wa madini kwenye maeneo ya misitu, endapo utajiridhisha kuwa uchimbaji huo unaathiri Ikolojia ya misitu hiyo.

Profesa SILAYO ametoa kauli hiyo mkoani Katavi baada ya kubaini kuwa,wachimbaji wengi wa madini wamekua wakipewa vibali vya uchimbaji bila TFS kuwa na taarifa, hali inayochangia kuendelea kwa uharibifu wa mazingira.

Ameongeza kuwa katika maeneo ya misitu ambayo Ikolojia yake ni ngumu kurejeshwa, uchimbaji wa madini hautafanyika kabisa, kwa kuwa madini yakiwa chini ya ardhi yana mchango mkubwa wa kutunza na kuhifadhi mazingira na Ikolojia yake.

Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa nchini, ambayo wachimbaji wake wa madini wamekuwa wakichimba madini hayo katika maeneo ya misitu, misitu iliyo
chini ya uangalizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini – TFS.