Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufanyika kama ilivyopangwa

0
196

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara amesema kuwa, uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika kama ilivyopangwa Novemba 24 mwaka huu licha ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutangaza kutoshiriki katika uchaguzi huo.

Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri Waitara amewataka Watanzania wote waliojiandikisha kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi huo pamoja na Vyama vyote vya siasa vinavyoendelea na mchakato wa uchaguzi, kuendelea na maandalizi kama kawaida.