Uchaguzi Arumeru Mashariki kufanyika Mei 19

0
543

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage ametangaza kuwa uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki utafanyika Mei 19 mwaka huu.

Tangazo la Jaji Kaijage limekuja siku chache baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kukubaliana na uamuzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, – Job Ndugai kutangaza kuwa Joshua Nassari amepoteza sifa za kuwa mbunge wa jimbo hilo.