Ubalozi wa Marekani watoa fursa kwa walimu

0
287

Ubalozi wa Marekani hapa nchini umetoa fursa kwa walimu wa somo la Kiingereza wanaofundisha shule za sekondari nchini kwenda na kufundisha nchini Marekani kwa wiki sita.

Programu hiyo ya mabadilishano inayoitwa Fulbright Teaching Excellence and Achievement (TEA) ni kwa ajili ya walimu wa Kiingereza wenye uzoefu wa miaka mitano au zaidi wa kufundisha ambapo kwa mwaka 2022/2023 ubalozi huo bado unapokea maombi.

Taarifa ya ubalozi huo imeeleza mwisho wa kupokea maombi hayo ni tarehe 13 Machi 2022