Wakati zoezi la uandikishaji Wananchi katika Daftari la Wapiga Kura likiendelea katika maeneo mbalimbali nchini, Rais John Magufuli na Mkewe Janeth Magufuli wamejiandikisha huko Chamwino mkoani Dodoma.
Rais Magufuli ambaye amemaliza ziara yake mkoani Katavi asubuhi ya leo, aliondoka mkoani humo na kuelekea mkoani Dodoma ajili ya kujiandikisha katika Daftari hilo la Wapiga Kura.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika Novemba 24 mwaka huu, ambapo Wananchi watakaoshiriki ni wale tu waliojindikisha katika Daftari hilo.
