Tupo tayari kusimamia maelekezo ya Rais

0
94

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuahidi Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ofisi yake ipo tayari kusimamia na kutekeleza maagizo yote ambayo Rais, atayatoa wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu hapa nchini.

Waziri Mkuu ametoa ahadi hiyo wakati akitoa salamu za ofisi yake katika mkutano huo unaofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mbali na kukutana na viongozi hao, mkutano huo pia utapokea maamuzi ya Serikali kuhusiana na mapendekezo yaliyotolewa na Kikosi Kazi kuhusu ufanyaji wa shughuli za kisiasa nchini.