Tupewe Elimu Kuhusu Mikopo

0
113

Katibu wa soko la Buguruni mkoani Dar es Salaam, Furahisha Kambi ameziomba taasisi zinazotoa mikopo kwa Wafanyabiashara kutoa elimu kuhusu mikopo kwa wafanyabiashara, ili waielewe na iweze kuwasaidia katika kuendesha biashara zao.

Kambi amesema wafanyabiashara wengi katika soko la Buguruni wamekuwa wakichukua mikopo ambayo hawaelewi masharti yake, hali inayoleta changamoto wakati wa kurejesha mikopo hiyo.

Amesema idadi kubwa ya wafanyabiashara wa soko hilo la Buguruni wanaochukua mikopo inayotolewa na halmashauri ni Mama lishe ambao wapo kwenye vikundi mbalimbali.

Kambi ameyasema hayo wakati wa kipindi cha Mirindimo ya Asubuhi cha TBC Taifa, kilichokuwa mbashara kutoka soko la Buguruni mkoani Dar es Salaam.