Tundu Lissu : Shirikianeni na Rais Samia

0
190

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa upande wa Bara Tundu Lissu, amewataka wanachama wa chama hicho kushirikiana na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye masuala mbalimbali yenye maslahi ya Taifa.

Lissu ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara kwenye uwanja wa Buliaga wilayani Temeke, Dar es Salaam alioufanya mara baada ya kurejea nchini akitokea Ubelgiji.

Amesema CHADEMA ina kazi kubwa ya kuhamasisha watanzania kuhusu maboresho ya sheria zilizopitwa na wakati , Ili kuendana na mazingira yaliyopo sasa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amewataka wadau wote wa siasa kushirikiana katika kuisimamia serikali ili iweze kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya.