Tulia: Suala la Bunge Live tutaliangalia

0
150

Spika wa Bunge la  Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa suala la matangazo ya bunge kuruka mbashara linazungumzika, na kwamba wataangalia kwanini liliondolewa na umuhimu wake kurejeshwa sasa.

Amesema Bunge kuwa live ni kitu kizuri, lakini lazima pia waone ni nini ambacho kinapelekwa huko kwa wananchi.

Amesema atazungumza na Waziri wa Habari pamoja na waandishi ili kupata maoni yao kabla ya kufanya uamuzi wa jambo hilo.