Tukio la kuvalishana pete lalaaniwa

0
127

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Zanzibar kupitia Kamisheni ya Utalii, imelaani kitendo cha watu wawili wa jinsia moja kuvishana pete katika ufukwe wa hoteli moja iliyopo Jambiani mkoa wa Kusini Unguja, na kusema uchunguzi unaendelea na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote walioandaa, kusimamia na kuhusika na tukio hilo ambalo ni kinyume na maadili na utamaduni wa Kizanzibar.

“Tunatoa onyo kwamba vitendo kama hivyo havitovumiliwa, kilichofanyika ni kinyume na sheria mbalimbali za Zanzibar ikiwemo sheria ya utalii ya Zanzibar namba 6 ya mwaka 2009 kifungu cha 27 (2), tunaomba Wananchi wawe watulivu wakati vyombo husika vikiendelea na hatua stahiki.” imeeleza taarifa ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar

Tarehe 20 mwezi huu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilipokea taarifa kuhusu tukio hilo baada ya picha ya video kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.