Tufanye biashara saa 24

0
173

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamilla kufanyia kazi wazo la kuwepo kwa eneo la biashara saa 24 siku zote za juma mkoani humo, ili kujiweka kwenye ramani nzuri kibiashara Kimataifa.

Majaliwa ametoa agizo hilo mkoani Dar es Salaam wakati akifungua rasmi Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2023.