Tudumishe amani yetu

0
122

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasihi na kuwasisitiza waumini wa dini ya kiislamu na Watanzania wote kudumisha amani iliyopo nchini bila kujali tofauti za kiitikadi, kikanda, kidini na kikabila.

“Amani inatufanya tuendelee kufanya ibada bila shaka yeyote ile, amani imetuwezesha kufanya shughuli za kutafuta riziki bila bughuba yeyote, Watoto watasoma na kila kitu kitaendelea kwa utulivu kutokana na amani tuliyonayo. Nchi nyingine hawana hicho kitu, hawawezi kukutana masaa yote, kila mmoja anawaza kwamba wakati wowote linaweza kutokea lolote lakini sio Tanzania”. Amesema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza kuwa

“Siri ya amani iliyopo nchini imetokana na uwepo wa dini zinazofundisha imani, zinazosisitiza amani na mshikamano”.

Waziri Mkuu Majaliwa alikuwa akizungumza katika Baraza la Eid Al Adha kitaifa lililofanyika katika Msikiti wa Mohammed VI Kinondoni, Dar es Salaam.