Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imetakiwa kuongeza jitihada katika kubuni programu mbalimbali za kutangaza vivutio vya Utalii.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana, wakati alipokutana na Menejimenti ya Bodi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Chana ameeleza kuwa licha ya TTB kuwa na jitihada za kuhamasisha utalii bado jitihada hizo haziendani na utajiri Mkubwa wa mazao ya Utalii yaliyopo Tanzania.
Ameongeza kuwa, ipo haja kwa Bodi hiyo kuongeza nguvu kuelimisha umma juu ya umuhimu wao kushiriki kikamilifu katika masuala ya Utalii.
Akielezea Mafanikio mbalimbali yaliyotokana na utendaji wa Bodi hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa TTB Felix John amesema kuwa ni pamoja na kuongeza Masoko katika nchi mbalimbali kama China, Urusi, India, nchi za Kiarabu na Ulaya.