TRAMPA yaitambua TBC

0
260

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limepatiwa cheti cha shukrani ikiwa ni kutambua mchango wake katika kufanikisha mkutano mkuu wa 10 wa chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu ya Nyaraka Tanzania (TRAMPA).

Cheti hicho kimekabidhiwa kwa TBC na Rais Samia Suluhu Hassan aliyefungua rasmi mkutano huo na kupokelewa na Anna Kwambaza ambaye ni Mkuu wa TBC Kanda ya Kaskazini.