TPSF wamlilia Dkt Mengi

0
266

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) Salum Shamte ametoa wito kwa Watanzania wote kufuata mazuri yaliyofanywa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Marehemu Dkt Reginald Mengi wakati wa uhai wake.

Shamte ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam, wakati akitoa salamu za TPSF kwenye shughuli ya kuuaga mwili wa Dkt Mengi katika Ukumbi wa Karimjee.

Amesema kuwa TPSF itaenzi mazuri yote yaliyofanywa na Dkt Mengi hasa katika kuwainua Wajasiriamali.

Shughuli ya kuaga mwili wa Dkt Mengi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais John Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja Wananchi mbalimbali.