Makampuni mbalimbali yameonesha nia ya kutaka kuja kuwekeza Katika Sekta ya mafuta na Gesi asilia hapa Tanzania baada ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan falme za kiarabu kwenye maadhimisho ya Siku ya Tanzania Expo 2020 Dubai
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC Dkt. James Mataragio wakati akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani Dar es salaam akieleza mafanikio ya maadhimisho hayo Katika Sekta ya mafuta na Gesi
“Kama Wadau wa Sekta ya mafuta na Gesi asilia tulikuwa na kikao kilichojumuisha Wadau zaidi ya mia mbili na wengi wa washiriki hao walionesha shauku (interest) ya kuja kuwekeza Tanzania kwenye maeneo ya usambazji wa Gesi, kujenga vituo vya kushindilia gesi kwenye magari na majumbani na kujenga mabomba ndani na nje ya Nchi”
“Kampuni zingine zilionesha nia yakuwekeza maeneo ya utafutaji gesi Katika mkondo wa juu na mkondo wa kati. Huku kampuni zingine zilionesha nia ya kuwekeza Ujenzi wa viwanda vya mbolea, viwanda vya kuchakata na kusafirisha Gesi (LNG) lakini pia kulikuwa na intereste kwenye maeneo yote ya Sekta ya Nishati” ameeleza Dkt. Mataragio
Aidha Mataragio ameongeza kuwa katika maonesho hayo TPDC imefanikiwa kusaini hati ya mashirikiano (MOU) na kampuni ya ADNOC ambayo inajihusisha na mafuta Nchini Abu Dhabi kama TPDC inavyohusika na utafiti wa mafuta Katika mkondo wa juu, kati na chini.
Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza viongozi, wafanya Biashara na watanzania mbalimbali Katika Siku ya Tanzania Expo 2020 Dubai huku Tanzania ikifanikiwa Kusaini mikataba mbalimba takribani 36 yenye thamani ya Trilioni 17 huku kukitarajiwa kuzalishwa ajira zaidi ya laki mbili.