TPDC kuzalisha zaidi Gesi asilia

0
121

Francis Lupokela Ofisa Uhusiano Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) akiwasilisha mada ya umuhimu wa matumizi ya Gesi asilia na mafuta Nchini kwenye mkutano wa 106 wa mafunzo ya uandaaji wa vipindi vya Televisheni Redio na Mitandao ya Kijamii.

Lupokela amesema Gesi asilia inazalisha zaidi ya asilimia 60 ya umeme kwenye gridi ya Taifa na inatumika kwenye magari Kama (CNG) Kwa gharama na nafuu lakini pia Gesi asilia inatumika kupikia majumbani kama Nishati ya kupikia.

“Gesi asilia inatumika kwenye viwanda kama chanzo cha Nishati na malighafi, Viwanda vikubwa Kama vile Dangote, Twiga, Goodwill baadhi Tu vinatumia gesi asilia” ameongeza Lupokela

Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), yakishirikisha maofisa wa habari wa Wizara, Taasisi, Mashirika ya Umma, Idara na Halmashauri.