Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linatarajia kuanza kuuza gesi nje ya nchi, kutokana na maombi ya nchi hizo kutaka kununua gesi kutoka hapa nchini
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, – James Mataragio amezitaja nchi ambazo ziko tayari kununua gesi ya Tanzania kuwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Malawi, Msumbiji na Zambia.
Akizungumza katika siku ya Pili ya Kongamano la Wadau wa Mafuta na Gesi, Mataragio amesema kuwa, kwa sasa TPDC inaangalia kwanza kiwango cha gesi kinachohitajika kwa matumizi ya nchi ili kitakachobakia iweze kukiuza kwa nchi zingine.
